Posts

KWA VILE KIMEKUSHINDA, HAIMANISHI KUWA HAUWEZI !!

    Nakumbuka ilikuwa ni tar 29/9 mwaka huu, nilipoamka asubuhi, nikiwa ninawaza juu ya baadhi ya mambo ambayo niliyafanya lakini nikashindwa. Nikawa najiuliza ni kwanini nilishindwa ? Je ni kwa vile yale mambo hayawezekani ? Nikasikia sauti ndani yangu inaniambia sio kwamba hayawezekani, kuwezakana yanawezekana ila uwezo wako ni mdogo. Unachotakiwa kufanya ni kuongeza uwezo sawa na neno la Mungu linavyosema “Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo”. (Mithali 24:5)  Ile sauti ikaendelea kunifundisha, ikaniambia kuwa kulikuwa na watoto wa 3 wa mfalme ambao walikuwa ni mapacha, na mfalme alikuwa anataka mmoja kati ya hao watoto wa 3 arithi kiti chake cha ufalme. Akawapa mtihani wa kubeba mzigo uliokuwa na kilo 300 na kuuweka juu ya ukuta ambao ulikuwa na urefu wa futi 4 kutoka ardhini. Na aliwapa muda wa mwaka mmoja na nusu wawe wamekamilisha hilo zoezi.  Wale watoto wote walikuwa na urefu wa futi 6 kila mmoja na uzito unaolingana. Mtoto wa kwa...

Je, Ni sawa Kupiga picha ukiwa katika Maombi kisha unaituma kwenye mtandao?

 Bwana Yesu alisema: “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. (Mathayo 6 : 6). Siku hizi mtu anakuwa kwenye maombi, anapigwa picha kisha anairusha kwenye mtandao na kutangaza kwamba alikuwa mbele za Mungu, au anaandika alikuwa anabubujika!! Mwingine anaamua kufanya maombi ya Kufunga, anakwenda Mlimani, halafu anakuwa anapiga picha kila siku, akiwa huko mlimani na kuzituma katika mtandao. Nini maoni yako kuhusu suala hili??

Aliyeko Juu Mngoje Chini!

 “Aliyeko juu mngoje chini”?  Hii ni methali ya kipepo kabisa. Ambaye anaitendea kazi mithali hii ataendelea kubaki chini akiwasubiria walioko juu kiuchumi, walioko juu kielimu, walioko juu kiroho, walioko juu kiufahamu, washuke chini. Na wasiposhuka chini atafanya kila njia awashushe ikibidi kuwaendea kwa waganga wa kienyeji na wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kufunga na kuomba ili hao walio juu yake washuke chini. Badala ya kujifunza kutoka kwao mbinu zilizowazesha wao kufika juu ili ajue wamefikaje hapo walipo; yeye anatafuta mbinu za kumsaidia awashushe chini !!   Watu wa jinsi hii ndio wale ambao hufurahia wakiona jirani yake kafukuzwa kazi utasikia: “HALO HALOO… WALIKUWA WANAJIDAI KULA WALI NYAMA, SIJUI WALI MAINI, SIJUI MARA LEO KITIMOTO, TUWAONE SASA KAMA WATATULINGISHIA TENA HIVYO VYAKULA VYAO”. YAANI WENZAO KULA VYAKULA VINONO WANAONA WANALINGISHIWA !!   Watu wa jinsi hii ndio wale ambao wakiona mfanyakazi mwenzake kapandishwa cheo wanamwendea kwa mganga ...

Kufurahia thawabu ya kashfa ya uongo

  Amini usiamini! Kumbe kuna thawabu kwa ajili ya kutungiwa kashfa za uongo! Haya si maneno yangu binafsi. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyesema haya kama ilivyoandikwa hapa chini: “Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.” (MT.5:11-12) Maneno mazito ni haya ya “watakapowashutumu…….na kuwaudhi……..na kuwanenea……. Kila NENO BAYA kwa UONGO….” Kuna kushutumiwa na kulaumiwa na kunenewa vibaya lakini kwa mambo ya kweli, kwa makosa ya kweli. Hii ni kawaida kila mkosaji kulaumiwa kwa makosa yake. Lakini si rahisi, na si kawaida, mtu asiye na hatia kabisa, kushutumiwa, kulaumiwa na kunenwa vibaya kwa tuhuma za kashfa za uongo. Tena tuhuma ambazo wahusika wanaweka mikakati ya makusudi huku wamepania kwa makusudi kumdhalilisha, kumvunjia heshima yake, huyo asiye na hatia “maskini wa Mungu” ili tu aabike, aadhirik...

Tuukomboe Wakati

  Waefeso 5:16-17. “mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”. “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana” Shalom. Leo tutafakari mambo machache tunapojiandaa kupokea mwaka 2017. 1. Tusiupokee mwaka kwa mazoea bali tujitafakari. Ukweli ni kwamba dunia inaingia 2017 lakini kifikra sio kila nchi au mtu amefika 2017. Kuna wengine muda wao umetekwa na hivyo hata 2016 kifikra bado hawajafika lakini wataupokea mwaka 2017 kimazoea tu na hawataona tofauti ktk maisha yao. Tunapaswa kuukomboa muda ambao adui ameuteka tukajikuta hatujafanya yale yaliyopasa. Mfano mtu mlevi au mzinzi hawezi kufanya mambo na maamuzi sahihi maana anaishi muda tofauti na hali halisi. Unaweza kumkuta mtu ana miaka zaidi ya 40 lakini bado hajaoa anaendekeza zinaa tu. Maana yake muda wake ktk eneo la ndoa umetekwa. Mtu kama huyo anahitaji maombi ya kumfungua ili aweze kuukomboa huo muda. Ndio maana tunaona pia maendeleo ni tofauti baina ya mtu na mtu. Yule mtu anayeishi kw...

Ukishindwa, Ongeza Uwezo!

  Nakumbuka ilikuwa ni tar 29/9 mwaka huu, nilipoamka asubuhi, nikiwa ninawaza juu ya baadhi ya mambo ambayo niliyafanya lakini nikashindwa. Nikawa najiuliza ni kwanini nilishindwa ? Je ni kwa vile yale mambo hayawezekani ? Nikasikia sauti ndani yangu inaniambia sio kwamba hayawezekani, kuwezakana yanawezekana ila uwezo wako ni mdogo. Unachotakiwa kufanya ni kuongeza uwezo sawa na neno la Mungu linavyosema “Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo”. (Mithali 24:5)  Ile sauti ikaendelea kunifundisha, ikaniambia kuwa kulikuwa na watoto wa 3 wa mfalme ambao walikuwa ni mapacha, na mfalme alikuwa anataka mmoja kati ya hao watoto wa 3 arithi kiti chake cha ufalme. Akawapa mtihani wa kubeba mzigo uliokuwa na kilo 300 na kuuweka juu ya ukuta ambao ulikuwa na urefu wa futi 4 kutoka ardhini. Na aliwapa muda wa mwaka mmoja na nusu wawe wamekamilisha hilo zoezi.  Wale watoto wote walikuwa na urefu wa futi 6 kila mmoja na uzito unaolingana. Mtoto wa kwanza ali...

Bwana Yesu Hajawahi Kushindwa

 Siku zote, tunaposhindwa, tunapoanguka, tunapoumia na kudharauliwa..  Tusisahau hatuko peke yetu katika kila hatua, Bali tunaye Bwana wa Mabwana, mfalme wa wafalme, jemedari mkuu,  Bwana wa Vita, hatatuacha tupigane peke yetu! Hajawahi na kamwe haitatokea akashindwa. Ni jambo gani la kumshinda huyu Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka na Yakobo?  HAKUNA Ni yeye Yule Jana, Leo na hata milele Waebrania 13:8 Mbarikiwe wapendwa, asanteni kwa kuendelea kufuatilia hapa..