Je, Ni sawa Kupiga picha ukiwa katika Maombi kisha unaituma kwenye mtandao?
Bwana Yesu alisema:
“Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. (Mathayo 6 : 6).
Siku hizi mtu anakuwa kwenye maombi, anapigwa picha kisha anairusha kwenye mtandao na kutangaza kwamba alikuwa mbele za Mungu, au anaandika alikuwa anabubujika!!
Mwingine anaamua kufanya maombi ya Kufunga, anakwenda Mlimani, halafu anakuwa anapiga picha kila siku, akiwa huko mlimani na kuzituma katika mtandao.
Nini maoni yako kuhusu suala hili??
Comments
Post a Comment